Joseph Kony (alizaliwa mwaka 1961 hivi) ni kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Lord's Resistance Army (LRA), ambalo limejihusisha na kampeni za ghasia likiwa na azma ya kuanzisha serikali inyoongozwa na viongozi wa dini nchini Uganda, kundi hili liandai limejengeka kwenye misingi ya Biblia ya Kikristo na amri kumi. Kundi la LRA ambalo lilijulikana kwa vitendo vyake dhidi ya wenyeji wa Uganda Kaskazini, limeteka nyara takribani watoto 30,000 na kusababisha watu milioni 1.6 kukimbia makazi yao tangu uasi wao ulipoanza mwaka 1986. [1] [2] [3]
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search